6/22/2022

Miss Brazil Afariki Dunia Baada ya Kufanyiwa Upasuaji wa Kuongeza Urembo

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Aliyekuwa Miss Brazil mwaka 2018, mrembo Gleycy Correia (27), amefariki Dunia Juni 20 baada kufanyiwa upasuaji wa kutoa mafindofindo.

Imeelezwa kuwa alipatwa na kiharusi na mshtuko wa moyo baada ya upasuaji huo ambapo alitokwa na damu nyingi.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa mrembo huyo alikaa kwa takribani miezi miwili kwenye moja ya hospitali huko nchini Brazil akiwa hajitambui baada ya upasuaji. Taarifa hiyo pia imetolewa na familia ya mrembo huyo.

Kiongozi wa kidini ambaye ni rafiki wa familia ya mrembo huyo, Mchungaji Jak Abreu, alieleza uchungu wake kwenye mitandao ya kijamii. Abreu alifichua kuwa wazazi wa mrembo huyo wanaamini kuwa kulikuwa na uzembe wa kimatibabu katika kesi yake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger