6/18/2022

MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, George Mpole Avunja Ukimya

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, George Mpole amewataka Watanzania kuthamini wachezaji wazawa tofauti na wanavyowachukulia.

Akizungumza na Mwanaspoti jana, Mpole alisema licha ya wao kutozungumzwa sana ila wanafanya kazi kubwa ingawa hawapewi sifa kama ambavyo wageni wamekuwa wakiimbwa kila siku.

“Watanzania wanapaswa kujifunza kuthamini vya kwao sina maana wageni hawafanyi mambo makubwa ila mzani ni lazima ubalansi licha ya ukweli wenyewe tunajifunza kutoka kwao,” alisema na kuongeza;

“Siongei kwangu binafsi ila ni kwa wazawa wote, wapo ambao wanaonyesha uwezo mkubwa kuliko hata hao wageni ila kwa bahati mbaya tunawasahau na kuthamini vya nje jambo tunalopaswa kubadilika.”

Mpole ndiye kinara mzawa mwenye mabao 15 kwenye Ligi Kuu Bara. Nyota wa Yanga, Fiston Mayele anaongoza msimamo wa wafunga akiwa na mabao 16.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger