6/15/2022

Msichana Akutwa na Mifuko 7 Aliyohifadhi Mabaki ya Mimba Alizotoa

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


 Mpangaji wa kike mwenye miaka 26 nchini Indonesia abainika kutoa mimba 7 kisha kuvifungafunga vijusi(foetuses) husika kwenye maboksi na mifuko na kuviacha humo humo ndani ya nyumba kwa miaka

Mwenye nyumba husika wa kike ndie amegundua hilo sasa baada ya mpangaji kuhama. Mpangaji husika ametambulishwa kwa herufi za mwanzo tu za majina yake N.M . Mwenye nyumba alipoenda kuangalia nyumba baadaye ili kuiweka katika hali ya usafi alikutana na harufu kali alipofuatilia inatokea wapi ndipo akabaini viumbe waliouliwa

Aliwataarifu polisi ambapo walimfuatilia mpangaji husika ambaye ni muajiriwa hospitalini, walimdaka na pia wamemkamata boyfriend wake

Baada ya kukamatwa na polisi akihojiwa amesema yeye na boyfriend wake walianza kutoa mimba hizo mwaka 2012 akiwa na miaka 16, na mara ya mwisho wametoa mimba mwaka 2021. Amesema alikuwa akinywa mchanganyiko wa madawa usioidhinishwa kisayansi ili kuchoropoa mimba husika kisha boyfriend wake kumsaidia kumuweka sawa mimba zote zitoke

Alipoulizwa kwanini walitoa mimba zote hizo amesema walikuwa wanaepuka unyanyapaa wa kuzaa kabla ya ndoa katika nchi hiyo inayoongoza kuwa na idadi kubwa zaidi ya waislamu duniani

Nchini Indonesia utoaji mimba ni kinyume na sheria labda tu kwasababu maalum zitakazobainika mfano mtu kubakwa

Hata hivyo, polisi bado wanajaribu kuchunguza zaidi kwanini wapenzi hao mimba zote walizotoa walizihifadhi ndani wanamoishi katika maboksi na mifuko badala ya kwenda kuzitupa au kwenda kuzifukia

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger