6/14/2022

Muigizaji Kajala Masanja Aliapa Akirudiana na Msanii Harmonize ‘Apigwe Mawe Afe’

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAMuigizaji Kajala Masanja.
Siyo stori tena kwamba, msanii Harmonize au Konde Boy na muigizaji Kajala Masanja wamerudiana.
Hii ni kutokana na matukio yanayoendelea baina ya wasanii hao wawili wa Tanzania hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Dalili kwamba tayari wametupa mzozo wao kwenye kaburi la sahau na kukubali kurudiana, zilianza kujitokeza wiki iliyopita wakati Kajala alipoondoa block ambayo alikuwa amemwekea Harmonize kwenye Instagram.
Harmonize pia alianza kumtambua Kajala kama ‘mke’ wake katika posti zake za Instagram ambazo zilimlenga mama huyo wa motto mmoja, Paula.

Takriban wiki mbili zilizopita Harmonize aliandika ujumbe wa pongezi kwa Kajala akidai kuwa alimpa motisha wa kufanya mazoezi.

“Asante kwa motisha mke. Dakika 23 kila siku na nahisi kama siyo kitu. Umenifanya kuwa mtu wa msaada na mvulana mzuri tena. Siwezi kusubiri kufanya mazoezi pamoja na wewe,” Harmonize aliandika chini ya video yake akifanya mazoezi.


 


Konde Boy aliendelea kumtaja Kajala kama mke wake katika posti zake nyingi kwenye mtandao huo.
Hatimaye wiki iliyopita, Kajala alijibu moja ya posti hizo za bosi huyo wa Lebo ya Konde Music Worldwide, jambo ambalo liliwasisimua wengi.

Katika posti hiyo, Harmonize alikuwa anampongeza Kajala kwa kusimama naye katika hali zote licha ya mabaya aliyomtendea.

Pia alithibitisha kuwa ni kweli alichorwa tattoo ya muigizaji huyo na binti yake Paula kwenye mguu wake wa kulia.

“Hakuna ambacho kitabadilisha kuwa nilikosea familia yangu. Hakuna ambacho kitabadilisha kuwa ni familia yangu. Pia hakuna ambacho kitabadilisha kuwa najivunia familia yangu mguu wangu wa kulia utasema sorry mpaka siku yangu ya mwisho… Nakupenda sana mke wangu Frida Kajala,” alisema Harmonize.


Ni wazi kuwa Kajala ambaye ndiye alikuwa mlengwa na aliweza kuona ujumbe huo, akausoma na kuupenda.
Baadaye Harmonize aliposti picha ya Kajala akiwa ndani ya nyumba ambayo inaaminika kuwa ni yake.
Staa huyo wa Bongo pia aliposti video nyingine ikionesha kabati lake la nguo na kusema kuwa imekuwa muda mrefu tangu lilipopangwa vizuri hivyo mara ya mwisho.


Harmonize.
“Sikumbuki mara ya mwisho kuona nguo zangu zikiwa zimepangwa vizuri hivi. Mapenzi yamenibadilisha kabisa, mimi ni mwanaume mpya. Asante mpenzi,” Harmonize alisema kuhusu video hiyo, maneno ambayo aliyekuwa akiambiwa ni Kajala.

Mmoja wa mameneja wa Harmonize, Choppa pia alifichua kuwa Kajala sasa ndiye bosi wa timu ya mameneja wake.
Choppa alimkaribisha Kajala katika timu yao na kusema kuwa anafurahia mno kufanya kazi naye.

“Niruhusu nimkaribishe katika timu ya usimamizi mkurugenzi na meneja mpya Frida Kajala. Nimefurahi kufanya kazi na wewe shem,” Choppa alisema.


 
Matukio haya ni dalili kuwa Kajala tayari amekubali msamaha wa Harmoniez na hata kukubali kurejesha mapenzi.
Hata hivyo bado hakuna yeyote kati yao aliyejitokeza wazi kutangaza hatua hiyo huku nyuma kukiwa na mjadala mzito wa kauli aliyowahi kuitoa Kajala mara baada ya kutengana na Harmonize.

Juma Lokole; ni rafiki mkubwa wa familia ya Kajala ambaye anadai kuwa aliongea na Kajala juu ya kurudiana na Harmonize ambapo alijiapiza kwamba never ever haitakuja kutokea yeye arudiane na Harmonize.
Jamaa huyo anaongeza kuwa, Kajala alisema kama ikitokea akarudiana na Harmonize, basi apigwe mawe mpaka afe!

Kwa upande wake, bintiye ambaye ni Paula alijiapiza kwamba, ni bora afe, lakini siyo kumuona Kajala akirudiana na Harmonize.

Watu wamepigwa na butwaa, wanajiuliza kulikoni?HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger