6/12/2022

Mume Amkata Kiganja Cha Mkono Mkewe Kisa Kapata Kazi Serikalini Huku yeye Muuza Genge

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mke huyo wa nchini India kwa jina la Renu amekatwa kiganja cha mkono na mume wake huyo kwa jina la Mohammad kisa ni mke kupata kazi serikalini


Mohammad yeye anamiliki kiosk(genge) cha kuuza vitu vidogo vodogo vya nyumbani kama mboga, matunda etc ila mke wake huyo alikuwa katika mafunzo ya unesi wakati huo huo akifanya kazi katika kituo binafsi cha afya


Sasa mke wake akapokea barua ya kuitwa kazini katika hospitali ya serikali ndio mume hajapenda akamkata mke wake kiganja ili asiweze kufanya kazi amtiii kwa kukaa tu nyumbani bila kazi


Tarehe 5 mwezi huu ndio mume akamziba mke wake na mto kisha kumfyeka kiganja ambapo mke alizimia, mume na wazazi wake wakampeleka hospitali na baada ya hapo wakatoweka hospitali, Renu alipoamka ndio akaona maisha yake tayari yamepewa ulemavu na mumePolisi walipofanya uchunguzi wamesema, kabla mohamad alikuwa hajiamini na aliwaambia marafiki zake kuwa anahisi Renu atamuacha baada ya kupata kazi serikalini hivyo atamfanya kitu


Baba mzazi wa Renu na Kaka wa Renu wakiongea kwa masikitiko wamesema walijua mume na wakwe wa Renu hawakutaka afanye kazi ingawa alikuwa anafanya kazi hata kabla ya ndoa lakini hawakudhani watamfanyia ukatili wa aina hiyo kukatisha ndoto zake baada ya kusoma kwa bidii miaka mitatu


Polisi bado wanamsaka mtuhumiwa na wazazi wa mume wote kusekwa lupango

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger