6/15/2022

Mwalimu Afa Kwa Moto, funguo za Nyumba zakutwa nje

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Mwalimu wa shule ya sekondari ya Morogoro Daudi Senyagwa, amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kutekea kwa moto akiwa amelala ndani usiku wa kuamkia leo Juni 15, 2022 katika mtaa wa Seminari, Kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro.

 

Wakizungumza na EATV mashuda wa tukio hilo akiwemo Mjumbe wa serikali ya mtaa huo Gregory Tandu, amesema alipigiwa simu majira ya saa 6:00 usiku kuwa kuna nyumba inawaka moto na walienda kujaribu kutoa msaada ilishindikana kwa kuwa walikuwa wachache na moto ulishakuwa mkubwa licha ya kukuta funguo ya nyumba hiyo ikiwa nje ya mlango.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela, amesema uchunguzi wa awali unaonesha kifo cha mwalimu huyo kimetokana na ajali ya moto baada ya kukuta viashilia vya mlipuko wa mtungi wa gesi lakini wataendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo ikiwemo mazingira ya funguo ya nyumba hiyo kuwa nje.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger