6/12/2022

Mwamba Amng'ata Pua MKEWE na Kuinyofoa Kisha Kukimba na Kutishia Kujiua

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Jamaa huyo kwa jina la Felix amemng'ata na kumnyofoa pua mke wake nyumbani kwa baba yake kisha kuibukia mtandaoni kutishia kujiua baada ya watu kumsema

Felix amezaa watoto 3 na mke wake huyo, lakini kwa mujibu wa taarifa Felix anadaiwa alikuwa hatulii ndani ya ndoa yake kwa kumsaliti mke wake huyo na wanawake mbalimbali na pia kumpiga mke wake mara kwa mara. Mwaka jana inadaiwa waligombana sana baada ya Felix kumtaka kimapenzi ndugu wa mke wake

Wanigeria hao, Ugomvi wao wa mara kwa mara ulipelekea mke huyo kuondoka na watoto kurudi kwa wazazi wake. Felix aliwaomba watu wa karibu wazungumze na mkewe amsamehe arudi waendelee kuishi pamoja

Baada ya kuombwa sana mke aliahidi tarehe 4 mwezi huu atarudi kwa mume, lakini siku husika Felix ndie alienda nyumbani kwa wazazi wa mke ambapo alipofika huko ugomvi uliibuka tena na kumng'ata pua mkewe na kuinyofoa kipande na kuondoka

Video ya mkewe huyo imesambaa mtandaoni akilia damu inamtoka mfululizo na sauti za watoto wao zinasikika kwa nyuma wakilia na kumuita mama yao


Baada ya video kusambaa watu walianza kumsema Felix ambapo aliibukia Facebook kuomba watu wamsamehe na kuomba mke wake pia amsamehe na kusema anawapenda watoto wake ataendelea kuwapenda hata akiwa hayupo duniani

Na katika ujumbe huo huo ametishia kujiua kwa madai ndani ya miezi mitatu hii akili yake haipo sawa amekuwa akipitia mambo magumu


Felix ametenda tukio hilo ikiwa ni wiki moja baada ya kumtakia happy birthday mkewe na kumwagia sifa za kila aina kuwa ni mke bora wakati akiendelea kumshawishi amsamehe arudi waendelee kuishi pamoja

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger