6/09/2022

Mwijaku: Ndio niliongea na Diamond nilikuwa namuuliza yeye amepewa kiasi gani na Wasafi bet maana mimi na yeye ni mabalozi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAMtangazaji huyo wa Clouds FM ameeleza kuwa yeye hayupo Upande wa Diamond na kuwa hata safari ya Mwanza hakupelekwa na Diamond bali alipelekwa na Wasafi bet kwa sababu wote ni mabalozi wa kampuni hiyo ya kubet.

Mwijaku anasema wakati yupo Mwanza na @diamondplatnumz alimuuliza yeye kalipwa bei gani maana wote ni mabalozi.”Ni kweli niliongea naye na nilikuwa namuuliza yeye kama balozi mwenzangu amelipwa kiasi gani Wasafi bet ? sikuongea naye chochote , Mimi ni balozi wa Wasafi bet, Diamond balozi wa Wasafi bet na Babalevo pia.”

Mwijaku amehoji kuwa kama Diamond angekuwa na hela ndugu zake wasingekuwa na shida huku akimtolea mfano Ricardo Momo kuwa alimuomba hela ya Luku Tsh 20,000.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger