6/07/2022

Mwimbaji nyota wa muziki nchini Zuchu Atangaza Kuachia Ngoma Mbili Kwa Mpigo

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Mwimbaji nyota wa muziki nchini @officialzuchu ametangaza ujio wa kazi zake mbili kwa pamoja yaani Double Release ifikapo Juni 24, 2022.


#Zuchu amebainisha ujio wa kazi hizo mbili kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo amesema moja kati ya nyimbo hizo 2 ni pamoja na "Jaro" wimbo ambao aliutumbuiza kwa mara ya kwanza kwenye tamasha la African Day huko Nigeria.


"Kwahiyo mashabiki wangu kuweni na utulivu, JARO yenu yaja na moto mwingine juu" - ameeleza @officialzuchu kwenye moja ya tweet yake.


Ikumbukwe, huu unaenda kuwa ujio wa pili kwa Zuchu kuuachia mwaka huu, mara ya mwisho kuachia nyimbo ilikuwa ni mwezi Februari ambapo aliachia wimbo uitwao "Mwambieni"


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger