6/01/2022

Nape Awapigia Debe Watanzania Kumiliki Simu Janja Kwa Wingi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Dodoma. Serikali imeagiza Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na makampuni ya simu watafute njia rahisi itakayowawezesha Watanzania wengi kumiliki simu janja ikibidi wakopeshwe na kulipa kidogokidogo.

Agizo hilo limetolewa leo Juni Mosi 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Taknolojia ya Habari Nape Nnauye wakati akipokea taarifa ya maboresho kwa mtandao wa simu wa Vodacom katika kufanya maboresho ya utoaji huduma zao.

Waziri Nape amesema Serikali inalenga watu wengi kuwa watumiaji wa data ili kupata taarifa muhimu lakini akabainisha kuwa mfumo wa kupata huduma hiyo humtaka mtu awe na simu janja ambazo wengi wanashindwa kumiliki kwa sababu ya gharama zake.

Amesema mara nyingi Serikali imekuwa ikihimiza namna bora ya watu kufikishiwa mawasiliano sahihi kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma, lakini wengi wanatamani kupata huduma hizo ila wanakwamishwa na uwezo mdogo.


“Lazima tufikie huko, naagiza TCRA wakutane na kampuni zote za mawasiliano ili watengeneze mfumo madhubuti kwa watu kupata simu janja, na malipo yawe siyo ya kumuumiza mtu bali walipe kidogokidogo hadi deni linakwisha na simu inakuwa yake,” amesema Nape.

Kwa mujibu wa Waziri,awali Serikali ilikuja na mpango wa kuondoa kodi kwa simu janja lakini jambo hilo halikusaidia kwa kuwa kiwango kilichoondolewa kilikuwa ni kidogo jambo ambalo anaona halikuwa na tija kwa wananchi.

Waziri Nape ameonya tabia inayoendelea kwa watumiaji wa simu kuendelea kupokea jumbe ambazo huduma zake watu hawakuomba akasema inapaswa kukoma mara moja kwa kuwa imeendela kuwa na usumbufu mkubwa kwa watu.


Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Sitho Mdlalose amemweleza Waziri kuwa, timu yao ilizunguka katika mikoa kadhaa ya Tanzania na kubaini bado kuna changamoto kubwa kwa watumiaji wa mtandao wao hivyo wamejipanga kumaliza kelele hizo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger