6/03/2022

Nesi adakwa na kilo 174.77 za heroine Tabata Relini

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA),Gerald Musabila Kusaya amesema, mamlaka hiyo imemkamata nesi msaidizi, Bw.Salum Shaban mkazi wa Tabata Relini katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam akiwa na kilo 174.77 za Dawa za Kulevya aina ya Heroine.

Ameyasema hayo leo Ijumaa (Juni 3) wakati akitoa taarifa kuhusu mambo mbalimbali yaliyofanywa na mamlaka hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Mei, 2022.

“Bwana Salum Shaban ambaye ni nesi msaidizi katika zahanati moja huko Kariakoo alikamatwa Mei 12, 2022 nyumbani kwake huko Tabata Relini akiwa ameweka kilo 174.77 za dawa za kulevya zikiwa juu ya kitanda chake, huku yeye akiwa amelala chini,”amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger