Ngorongoro - Loliondo: Askari Polisi Amekufa Baada ya Kupigwa Mshale Mmoja, RC Mongella amlilia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Askari Polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa mshale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa zoezi la uwekaji mpaka katika eneo la pori tengefu kwenye Tarafa ya Loliondo.


Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema kwamba kifo hicho kilitokea Juni 10 alasiri, na kusisitiza kwamba kama serikali wanatambua uzalendo wa askari huyo.


Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.


Wananchi wanatakiwa na Serikali kuhama katika eneo la Ngorongoro na kwenda kuishi Handeni, Tanga ambapo Serikali itawasaidia katika kuhama. Nia ikiwa ni kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.


Baadhi ya Wananchi wa Ngorongoro hawataki kuhama katika ardhi yao ya asili kwani Wanaishi hapo kisheria na Wanatambulika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad