6/03/2022

Pablo afunguka kilichomng'oa Simba, awataja mastaa

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAKOCHA aliyepigwa chini na Simba juzi, Pablo Franco amefunguka kwa mara ya kwanza sababu zilizomsababisha apoteze kazi.

Pablo ambaye anarudi kwao Hispania wiki ijayo amesema kitendo cha kushindwa kuvuka robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika na kubeba ubingwa wa mashindano yote ya ndani ni tatizo.

“Kuna baadhi ya wachezaji katika timu walishindwa kuwa katika viwango bora kwenye wakati muhimu ambao timu inawahitaji na halikuwa jambo jema kwetu na tulishindwa kufanya vizuri katika michezo hiyo,” aliongeza Pablo.

“Kuna ugeni wa mazingira yalikuwa changamoto na kushindwa kufanya vizuri katika baadhi ya mechi kama malengo ya timu yalivyokuwa


 
“Kuanza msimu katikati pia ni tatizo. Nilipambana nalo kutokana na mazingira yalivyokuwa ila kwa kiasi kikubwa hatukufanikiwa kama nilivyokuwa nikihitaji.

“Kikosi kilikuwa na wachezaji wengi wenye majeraha tena wale wa kikosi cha kwanza ilikuwa ngumu kwetu ila tulipambana kutokana na mazingira yalivyokuwa hadi kutumia wengine ambao kiasili sio nafasi zao.

“Kuna changamoto ya ratiba kucheza mechi kila baada ya siku chache jambo ambalo lilikuwa linatupa wakati mgumu kwani tulikuwa na mashindano mengi kwa wakati mmoja tofauti na wenzetu.”


Kikosi cha Simba kitarejea kambini Juni 6, kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu Bara ambayo imesalia na Pablo kabla ya kuondoka nchini atakwenda kambini kuwaaga wachezaji pamoja na wasaidizi wake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger