6/11/2022

Paula Kajala Amsamehe Mama yake Kurudiana na Harmonize

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


PAULA Kajala; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania na ni binti wa mastaa, mwigizaji Kajala Masanja na prodyzua P Funk Majani ambaye wakati msanii wa Bongo Fleva, Harmonize au Konde Boy akiomba kurudiana na mama yake, aliapa kwamba kama itatokea hivyo, labda awe amekufa.

Hata hivyo, mtoto hakui kwa mzazi wake na hicho ndicho kimejiri kwa Paula au Pau ambaye amesalimu amri kwa mama yake kisha kumsamehe kwa kitendo chake cha kurudiana na Harmonize.


Mara tu baada ya kusikia mama yake amerudiana na jamaa huyo, Paula aliamua kutomfuata mzazi wake huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kum-block kabisa, lakini sasa amelegeza kamba.


Taarifa za ndani kabisa zilizolifikia Gazeti la IJUMAA kutoka wa vyanzo vyake vya karibu na familia hiyo zimeeleza kuwa, ni rasmi sasa Paula amemsamehe mama yake na maisha yanaendelea.


Imeelezwa kwamba, Paula ameyakubali mahusiano ya mama yake na kumtaka awe huru na Harmonize.


Hii ni baada ya Kajala kuendelea kushikilia msimamo wake wa kumrudia Harmonize na kukubali kupoteza hata watu wake wa karibu, lakini aendelee na maisha yake ya Konde Boy.


Watu wa karibu wamesema kuwa, ilikuwa ni lazima Paula akubali uamuzi wa mama yake na kutengua rasmi kile kiapo aliachoapa kwamba; “Labda nife!”


Katika sakata hilo, Kajala ameendelea kupokea lawama kama zote, lakini ameendelea kuwa imara huku akipewa magari ya kifahari aina ya Range Rover na kupewa cheo cha meneja kwenye Lebo ya Konde Gang inayomilikiwa na Harmonize.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

2 comments:

  1. Mtoto asijibebeshe majukumu yalio juu ya uwezo wake. Kamba ambavyo hakujichagulia baba ndivyo sasa hawezi mchagulia mama mume.

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger