6/07/2022

Polisi yamsaka Mume Anayedaiwa Kumuua Mkewe

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mkazi wa Mazizini Ukonga kwa tuhuma za kumuua mke wake, Logesara Chitemo kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Jumanne Muriro amesema tukio hilo lilitokea Juni 6, 2022 ambapo marehemu alikuwa anauza pombe ya kienyeji ndipo walianza ugomvi ambapo mume wake.

Amesema kuwa baada ya kuibuka ugomvi kati ya wawili hao, mume alimchoma mkewe na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha kifuani na kichwani na baadaye kufariki dunia.

Kamanda Muliro amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho alikimbia kusikojulikana.


"Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na lazima tutampata na tutamfikisha kwenye vyombo vya sheria,"amesema Muliro.

Ametoa rai kwa wananchi pale inapotokea migogoro kwenye familia kushirikisha ndugu au taasisi za kidini na vyombo vya kisheria kikiwamo ya ustawi wa jamii pamoja na mahakama ili kutatua migogoro hiyo.

Kamanda Muliro amesema oparesheni ya kuzuia vitendo vya uhalifu katika Jiji la Dar es Salaam inaendelea ambapo vikosi mbalimbali vukiwamo vya mbwa na farasi vinafanya doria maeneo ya Cocobeach, Cocomihogo na Coco Plaza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger