Rais Samia amng’ang’ania Jenerali Mabeyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema bado ataendelea kumpa majukumu Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo kwakuwa bado ana nguvu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ameyasema hay oleo Alhamisi tarehe 30 Juni 2022 kwenye hafla ya kumwapisha Mkuu Mpya wa Majeshi Jenrali Jacob Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Salum Othman.

“Kama nilivyokuambia jana unaacha ukiwa kijana bado una nguvu na kwa maana hiyo tutaendelea kukuteua, tutaendelea kukupa majukumu uendelee kutusaidia, nadhani jioni ya leo Katibu Mkuu kiongozi utasikia kwenye bomba tayari ameshakupangia kazi ya kufanya,” amesema Rais Samia.


Rais Samia amesema Jenerali Mabeyo amefanya kazi yake kwa uaminifu mkubwa “umetumikia cheo chako kwa jitihada kubwa na leo unamaliza na kukabidhi kwa wengine nakushukuru sana na nakupongeza sana kwasababu si kazi rahisi.”

Kwa upande wa CDF mpya Jenerali Mkunda na Mnadhimu Luteni Jenerali Othman, Rais Samia aliwapongeza na kuwatakiwa kazi njema na kwamba atazuungumza nao.

“Niwapongeze na niwatakie kazi njema mkaanze pale Jenerali Mabeyo alipoishia najua kwenye jeshi hakuna mtu kuingia na yake kama tulivyo kwenye Serikali-Rais Samia…maelekezo zaidi tutazungumza inbox kwa leo itoshe kuwapongeza na mfanye kazi kama aliyetoka na mkaendelee pale alipoishia,” amesema Samia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad