6/09/2022

Rais Samia: Nimevutiwa Sana na Ajira Niliyoikuta Hapa Kiwanda cha Sukari

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akongea na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema amevutiwa sana na kiwango cha ajira kilichotolewa na Kampuni ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera (Kagera Sugar).

Rais Samia ameyasema hayo wakati akiwahutubia wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa ziara yake kiwandani ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Kagera.

“Nimekuta vijana wetu waliohitimu vyuo mbalimbali wako hapa wanafanya kazi hapa, wanaeleza mambo makubwa na nimewashuhudia wakifanya mambo ambayo huko nyuma kiwanda hiki kingehitaji wataalam kutoka nje kuja kuelezea namna ya kufanya lakini leo yanafanywa hapa.”alisema Rais Samia


Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera
Aidha Rais Samia amesema kuwa ziara yake kwenye kiwanda hicho imekuwa na manufaa sana kwani ameweza kuona mwenyewe kwa macho yake changamoto alizokuwa akiambiwa ambazo awali alihisi kuwa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho alikuwa akilalamika tu.


Mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera
Rais Samia pia ametumia fursa hiyo kuipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda pamoja na Wafanyakazi wote wa Kiwanda hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia amebainisha kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alimdokeza kuwa sekta ya sukari inaonesha mfano mzuri wa ukuaji mwaka hadi mwaka.

Kwa upande mwingine Rais Samia amebainisha kuwa Serikali imetenga kiasi cha Bilioni 20 kwa ajili ya kuendeleza mashamba makubwa ikiwemo ya Miwa, Michikichi pamoja na Arizeti.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger