6/10/2022

Rappa Lil Nas X Awachana BET Kwa Kukosa Kumteua Kuwani Tuzo Mwaka Huu

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Rappa Lil Nas X ameachia wimbo mpya ambao anawachana waandaaji wa tuzo za BET kwa kukosa kuteuliwa kuwania tuzo hizo mwaka huu pamoja na kutotumbuiza kwenye hafla ya usiku wa utoaji wake.

Rappa huyo ambaye jina lake halisi ni Montero Lamar Hill, aliposti kipande cha video kinacho muonesha akiimba wimbo huo kwenye akaunti yake ya Twitter akiwachana mbaya mbovu.

Ikumbukwe, waandaaji wa tuzo za BET yaani Black Entertainment Television Awards walitoa orodha ya walioteuliwa kuwania tuzo hizo siku ya Juni Mosi, lakini Lil Nas X sio mmoja wao.

Lil Nas alionyesha kutoridhika kwake kupitia ujumbe ambao aliandika na kufuta kwenye ukurasa wake wa Twitter, “Thank you BET Awards. An outstanding zero nominations again. Black excellence!” yaani, “Asanteni tuzo za BET. Sijapokea uteuzi wowote tena. Ubora wa watu weusi.”

Kwenye wimbo wake Lil Nas anasikika akitusi tuzo hizo na kuwaambia waandaaji wasimjaribu. Hata hivyo, waandaaji wa BET nao kupitia ukurasa wao wa twitter wamejibu juu ya wimbo huo wa Lil Nas X.

BET wameeleza wanampenda sana kama msanii na wakafafanua kwamba hakuna yeyote kutoka BET ambaye anahusika kwa kuteua wawaniaji wa tuzo hizo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger