Ticker

6/recent/ticker-posts

Rayvanny Ametupiga na Kitu Kizito Kichwani...Hakuna Shirika la Ndege Linalofuta Safari zake Kwa Ajili ya Mtu Binafsi Kushoot Video


Ni ngumu kujua Rayvanny anataka nini kwenye muziki, kuwa appreciated ama kuacha legacy kwenye anacho kifanya, Ubaya zaidi vyote viwili huwezi kuvipata ukiwa muongo kwa walaji wa kazi zako.

Kuchoma vitu, wataalamu wa motion graphics wanaweza eleza ni kwa namna gani teknolojia inaweza fanya hilo, lakini pia si sababu za kutaka kuuaminisha umma kuwa video flani ni gharama, kingine Video ya Tequiero haiendani kabisa na maudhui ya wimbo, hadi mtu unajiuliza lengo lilikuwa kushoot filamu au Music Video?

Kingine hakuna shirika la ndege duniani kote linaweza futa safari ya ndege yake kisa kuna mtu kakodi ndege hiyo kwaajili ya kushoot Music Video ama Filamu, Rayvanny kadanganya kweupe, hajui ni adhabu gani hilo shirika linaweza kutana nayo ikiwa hilo litatokea, shirika litaghairi safari yake kwa sababu za Hali ya hewa, usalama na vitu vichache sensitive.

Video nzima gharama yake ni 100M, ondoa kuchoma moto Alteza (kwa mujibu wake), kukodi kirikuu kwaajili ya magaidišŸ˜, unakodi ndege kwa siku nzima kwa shillings ngapi? Na hiyo ndege kwa safari moja inaingiza kiasi gani? Hao abiria wanaosafiri wanaenda kulala huko destination au wana majukumu yao?

Wasanii wa Bongo wanafake sana, wakiambiwa ukweli wanatembeza BlockšŸ¤£.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments