Sabaya Amkataa Mwendesha Mashtaka Moshi Kisa Anatoka Hai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, amemkataa Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tumaniel Kweka kwa kuwa anatokea wilaya ya Hai.

Aliwasilisha hoja hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Salome Mshasha, Sabaya alisema hana imani na mwendesha mashitaka huyo kwa kuwa anatokea katika wilaya hiyo na kwamba ni mtu aliyedai ni wa visasi na anatumika kisiasa.

Sabaya na washtakiwa wenzake wanne wanaokabiliwa na mashitaka saba ambapo alienda mbali na kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kesi hiyo.

Mbali na hoja hiyo lakini kulijitokeza hoja nyingine kupitia kwa wakili Hellen Mahuna, aliyedai washitakiwa hao hawakupelekwa mahakamani hapo kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba mawakili wao hawakupewa taarifa.


Kutokana na malumbano hayo, Hakimu Mshasha ameahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 10 hadi 15 ili kupitia hoja hizo ili kutoa uamuzi mdogo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad