6/16/2022

Simba SC imeanza na Moses Phiri, yamtambulisha rasmi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Hatimaye Klabu ya Simba SC imemtangaza Kiungo Mshambulia kutoka nchini Zambia Moses Phiri kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo, ambaye rasmi ataanza kuonekana kikosini msimu mpya wa 2022/23.

Phiri anakua mchezaji wa kwanza kutambulishwa kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, kuelekea mwishoni mwa msimu huu 2021/22, huku akitarajiwa kufanya makubwa msimu ujao 2022/23.

Taarifa kutoka Simba SC zimeeleza kuwa, Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili ambao rasmi utafikia ukingoni mwa 2024.

Simba SC ilianza kuhusishwa na mpango wa kumsajili Phiri msimu uliopita, lakini ilishindikana kutokana na mkataba wake na klabu ya Zanaco FC, ambayo ameitumikia kwa zaidi ya miaka mitatu.


 
Young Africans nao walihusishwa na mpango wa kumsajili Mshambuliaji huyo mwezi Januari mwaka 2022, nao pia waligonga mwamba, kufuatia Uongozi wa Zanzco FC kuweka ngumu kwa kisingizio cha kuhitaji huduma yake kwenye michuano ya Kimataifa (Kombe la Shirikisho Barani Afrika).
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger