6/20/2022

Simba SC yaangukia kwa Josef Vukuzic mwenye UEFA PRO License A

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Uongozi wa Klabu ya Simba SC upo katika hatua za mwisho kumuajiri Kocha kutoka nchini Slovakia Josef Vukuzic mwenye UEFA PRO License A.


Inaelezwa kuwa mazungumzo ya pande hizo mbili yamefikia pazuri, na huenda mambo yakakamilika ndani ya juma hili, na Kocha huyo kutangazwa kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC.


Josef alianza kazi ya ukufunzi wa soka mwaka 1999, amezunguka katika vilabu mbalimbali takribani 13 na Barani Africa amefundisha vilabu 4 (Al ahly Benghazi, Cape Town City, Polokwane na Amazulu).


Mwaka 2018 alifundisha Polokwane City na kuwaongoza kumaliza katika nafasi ya tano akatimuliwa na kujiunga na Amazulu FC 2019, ambayo aliwaongoza katika Michezo 20 tu, na akaondoka huku sababu zikitajwa kutoelewana na wachezaji pamoja na matatizo ya COVID 19.


Kwa sasa Kocha Josef anakinoa kikosi cha klabu ya Kosice ya Slovakia, ambapo amekiongoza katika Michezo 33 akishinda mechi 19 akipata Sare 5 akipoteza 9.


Josef, anatumia mfumo wa 4-3-3 hajawahi kuipa klabu ya Africa Ubingwa wa Ligi na hata kufikisha hatua ya juu katika mashindano ya kimataifa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger