6/13/2022

Simba SC yamkana tena Stephen Aziz Ki

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Uongozi wa Klabu ya Simba SC umeendelea kukanusha taarifa za kutuma ofa ya kutaka kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Fasso na klabu ya ASEC Mimosas Stephen Aziz Ki, kama ilivyoripotiwa juzi Jumamosi (Juni 11), katika mitandao ya kijamii.

Simba SC ilihusishwa na mpango huo, huku barua ya ofa iliyokua na nembo la Simba SC ikisambazwa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, ikionyesha namna ilivyokua inamshawishi mchezaji huyo kujiunga Msimbazi msimu ujao.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema klabu yao haijawahi kutuma ofa ya aina yoyote ya kumsajili Aziz Ki, zaidi ya kuamini kilichofanywa ni kitendo cha kihuni kuihusisha klabu hiyo na mambo hayo.

“Simba SC hatujawahi kupeleka offer ya mkataba kwa Aziz Ki ni propaganda zimetengenezwa kwa ajili ya wanaomuitaji kuonesha kuwa wametupiga bao”

“Simba SC ina mipango yake, na ina taratibu zake za usajili, haiwezi kuanika wazi ofa inayotumwa kwa mchezaji ama klabu fulani, Simba SC imekua na usiri mkubwa sana katika usajili wake, tazama misimu iliyopita tumekua tukiwatambulisha wachezaji wetu kwa aina tofauti kabisa, kwa nini hii iwe hivi? Kuna makusudi imefanywa hapo na ndio maana tulikanusha kupitia mitandao hiyo hiyo ya Kijamii.”  Amesema Ahmed Ally

Simba SC imejipanga kufanya usajili mkubwa mwishoni mwa msimu huu, baada ya kushindwa kufikia malengo yake msimu huu 2021/22, kwa kupoteza mataji la Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, huku ikishindwa kuvuka hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger