Ticker

6/recent/ticker-posts

Sina Tatizo na CEO, Simba ikifungwa Naumia sana – MorrisonMchezaji wa Klabu ya Simba, Bernard Morrison amesema kuwa bado anaipenda timu hiyo na kama atapewa kile anachohitaji kwenye mkataba mpya basi atasalia hapo sababu anaipenda sana huku akiongeza kuwa hana matatizo yoyote na CEO, Barbara Gonzalez na sio kama inavyozungumzwa.


”Bado naipenda Simba, nawapenda watu wake, hivyo Simba inapocheza iwe imefungwa ama imepata sare najisikia vibaya (naumia) natamani kama niwepo pale na kutoa mchango wangu pengine tunaweza kushinda.” amesema Morrison.


Alipoulizwa kama ana matatizo yoyote na CEO, Barbara @bvrbvra nyota huyo amesema ”Kuna vitu vingi ambavyo watu hawavifahamu, CEO ni mtu wa siri, ni mtu mzuri sana, siwezi kusema nina matatizo na yeye. Kuna baadhi ya vitu ambavyo amenifanyia siwezi hata kuelezea maana hata yeye hajataka kuviweka hadharani watu wajue, hivyo kwa mimi kusema nina matatizo na CEO Barbara hapana na ni mtu anayeniheshimu na naamini maamuzi aliyochukua kuhusu kusimamishwa kwangu ni maamuzi ya Klabu kwa sababu yeye ndiyo CEO wa timu.”


Morrison ameongeza ”Kama nitapata simu ya CEO au Mwenyekiti wa Klabu na kuniambia watanipa ninachohitaji nitasaini mkataba. Kama Simba watanipa ninachohitaji na kusaini mkataba nitafurahi sana.”


Imeandikwa na @fumo255

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments