6/23/2022

Spika afuta maneno ya Waziri kwenye ansadi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson ameagiza maneno ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula dhidi ya Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi, kufutwa kwenye ansadi za Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Itakumbukwa kuwa juzi tarehe 21 Juni, 2022 bungeni hapo, Kunambi aliomba mwongozo wa Spika kuhusu maneno ya Dk. Mabula ambayo alidai yanamvunjia heshima endapo yanaruhusiwa na kama yanaruhusiwa athibitishe au afute kauli yake.

Dk. Mabula alisema kuwa mfano aliotoa mbunge huyo kuwa wakati akiwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma alisimamia vizuri upimaji wa viwanja, haufai kuwa mfano mzuri kwasababu ulikuwa wa dhuluma kwa wananchi na kuacha malalamiko mengi.

Mabula aliendelea kueleza kuwa hivi sasa Dodoma ndiyo inayoongoza kwa migogoro ya ardhi nchini ikiizidi Halmashauri ya Kinondoni ambayo ilikuwa kinara kwa muda mrefu.


 

Akitoa mwongozo wa suala hilo leo Alhamisi tarehe 23 Juni, 2022, Dk. Tulia alisema maneno aliyotoa Dk. Mabula dhidi ya Kunambi ni Kinyume na kanuni ya 76 ya Kanuni za kudumu za bunge na kwamba jambo hilo haliruhusiwi kwasababu linaingilia uhuru wa mawazo na majadiliano wa mbunge na inamvunjia heshima yake.

“Hayo si maneno yanayoruhusiwa katika mijadala ya bunge kwa mujibu wa kanuni ya 71 fasiri ya kwanza (i) na (j) zinazuia kumsema vibaya mbunge na matumizi yasiyo sahihi ya lugha ya kumdhalilisha mbunge,” amesema na kuendelea;

“Hivyo haikuwa sahihi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutamka kuwa ilikuwa dhuluma kwa wananchi endapo kuna dhuluma ilifanyika kuna vyombo vinavyohusika vinaweza kuchukunguza na kuchukua hatua stahiki zikachukuliwa.”


Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson
Dk. Tulia amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 76 ya Kanuni za kudumu za bunge maneno hayo hayaruhusiwi na haikuwa sahihi kwa Waziri kuyatamka.

“Hivyo naelekeza maneno yanayolalamikiwa yafutwe kwenye ansadi ya tarehe 21 Juni 2022 kwa mujibu wa kanuni ya 5 fasiri ya kwanza ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2020,” amehitimsha.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger