6/08/2022

Sure Boy Atoa Kauli ya Kibabe Yanga, Aaahidi Kuwaziba Watu Midomo

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAKIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ amekiri kukutana na ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi hicho, lakini kamwe hatakubali kukaa benchi na badala yake atapambania nafasi yake.

 

Staa huyo amekutana na ushindani wa namba wa viungo kutoka kwa Mganda, Khalid Aucho, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Yannick Bangala na Zawadi Mauya.

 

Sure Boy alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Azam FC baada ya kuomba mkataba wake uvunjwe.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Sure Boy alisema kabla ya kukubali kusaini Yanga, alifahamu ushindani atakaokwenda kukutana nao kutoka kwa viungo wa timu hiyo.


Yannick Bangala Litombo

Sure Boy alisema kuwa, licha ya kujihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mtunisia, Nasreddine Nabi, lakini bado hajaridhika, hivyo amepanga kuendelea kuonesha kiwango bora ili aendelee kucheza.

 

Aliongeza kuwa, kikubwa alichopanga ni kuendelea kufanya mazoezi ya binafsi ili kufanikisha malengo yake ya kuendelea kucheza kwa kiwango kizuri.


Khalid Aucho nyota kutoka Uganda

“Ngumu kwenda katika timu mpya bila ya kukutana na ushindani, hivyo wakati nachukua maamuzi ya kuja kuichezea Yanga nilifahamu kabisa nakwenda kukutana na ushindani wa viungo bora.

 

“Lipo wazi kabisa, Yanga ni kati ya timu iliyokuwa na viungo bora ambao ndio wameifanya timu ionekane bora na kukaa kileleni katika msimamo wa ligi.

 

“Nikizungumzia viwango bora katika ligi lazima uwataje Aucho, Bangala na Fei Toto ambao ndio wanawafanya mabeki wacheze bila ya presha kwa maana ya kutoshambuliwa kila wakati,” alisema Sure Boy.

WILBERT MOLANDI
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger