6/06/2022

Tanzania yaichapa Zanzibar 12-0

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


TIMU ya Twiga Stars inayowakilisha Tanzania Bara imeishushia Zanzibar Queens kichapo cha mbwa mwizi mabao 12-0 katika mchezo wa pili wa michuano ya Cecafa.

Tanzania Bara 'Twiga Stars' ilianza kutupa karata yake Jumapili ikiwafunga 2-0 Sudan Kusini huku Zanzibar Queens wakifungwa mabao 5-0 na Ethiopia.

Mchezo wa pili Kilimanjaro Queens ilitoka sare ya mabao 2-2  dhidi ya Ethiopia huku Zanzibar Queens ikiambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Sudan kusini.

Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jumamosi katika uwanja wa Jinja Nchini Uganda Kilimanjaro wakitamba katika kundi lao D.
Mabao ya Kilimanjaro Stars yametiwa kimiani na Oppa Clement aliyefunga manne akiondoka na mpira wake kibindoni.

Mbali na Oppah aliyeondoka na mpira hata Mwanahamis Omary naye amefunga mabao matatu pekee.

Mabao mengine yamefungwa na Janeth Pangamwene, Diana Msewa, Enekia Lunyamila, Protas Mbunde pamoja na Ester Mabanza.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger