TANZIA: Wanafunzi Watatu Udom Wafariki Ajali ya Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Dodoma. Wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana jioni katika moja ya barabara zilizopo chuoni hapo.


 Akizungumza leo Jumapili Juni 5, 2022 na Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrece Baltazar amesema ajali hiyo imetokea jana saa 2.00 usiku.


Amewataja waliofariki kuwa ni Hana Meshack, Zira Mpenda, Mpeli Mahenge.


Beatrece amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Fortunata Kingazi, Fibi Julius, Sifa Shora, Enica William na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Furahina.


Amesema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na hali zao zinaendelea vizuri.


Taarifa zinasema wanafunzi hao walikuwa wanatoka katika mahafali ya dini yaliyokuwa yakifanyika chuoni hapo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno ameahidi kutoa taarifa baadaye.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad