Urusi Yamhukumu Jela Miaka 14 Raia wa Marekani Kwa Kosa la Kukamatwa na Bangi


Matumizi ya bangi ni halali kwa baadhi ya maeneo nchini Marekani

RAIA wa mmoja wa Marekani anayefahamika kwa jina la Marc Fogel amehukumiwa kwenda jela miaka 14 nchini Urusi kwa kosa la kukamatwa na bangi.

Mahakama nchini humo imemtia nguvuni Fogel ambaye mwanzo aliwahi kufanya kazi katika Ubalozi wa Marekani nchini Urusi akiajiriwa kama Mwalimu wa somo la Kiingereza.

Fogel amefungwa kwa sheria ileile ambayo inasikiliza kesi nyingine ya mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu wa Marekani Brittney Griner, bangi ni halali kwa maeneo mengi ya Marekani lakini kwa Urusi bangi ni kinyume na sheria.

Taarifa kutoka Mahakama katika mji wa Khimki jijini Moscow imesema:

“Raia wa Marekani Fogel amekutwa na hatia.”

Fogel ambaye anakaribia umri wa miaka 60 alikamatwa na jumla ya kilo 17 za bangi katika mizigo yake mnamo Agosti 15, 2021 katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo.

Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia zinadai Fogel alikiri kutunza, kusafirisha, kuzalisha na kuandaa madawa hayo ya kulevya, na kama sehemu ya upelelezi Polisi walitoa picha alizopigwa Fogel wakati amefanyiwa msako katika shule aliyokuwa akifundisha jijini Moscow.

Biashara ya madawa ya kulevya pamoja na matumizi yake ni kinyume na sheria kwa mataifa mengi duniani

Tayari kuna raia kadhaa wa Marekani ambao wanatumikia kifungo katika magereza ya nchini Urusi akiwemo mwanajeshi wa vikosi vya majini Paul Whelan ambaye alipewa hukumu ya miaka 16 tangu mwaka 2020.

Marekani nayo inawashikilia baadhi ya raia wa Urusi ambapo mnamo mwezi wan ne mwaka huu nchi mbili zilikubaliana kubadilishana wafungwa ambapo mwanajeshi mstaafu wa vikosi vya majini wa Marekani alibadilishwa na rubani wa ndege wa Urusi ambaye alikuwa amefungwa tangu mwaka 2010.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad