6/14/2022

Video ya Wimbo "Jerusalema" Yaweka Rekodi Barani Afrika...Unaambiwa Hakuna Msanii Aliyefikia Kusini Mwa Jangwa la Sahara

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Video ya wimbo "Jerusalema" wake @masterkgsa iliyotoka Desemba 12, 2019 imefikisha views milioni 500 youtube tangu itoke miaka miwili iliyopita.


Hadi sasa "Jerusalema" ndio video iliyotazamwa zaidi katika mtandao wa youtube kusini mwa Jangwa la Sahara kwa muda wote.


Wimbo huo uliokuwa kileleni mwa chati nyingi za muziki duniani, ulishinda tuzo ya Best African Act (inayotokana na video yenye uchezaji bora wa muziki) katika tamasha la kutoa tuzo la MTV barani Ulaya Novemba mwaka 2020.


Mwimbaji wa ngoma hiyo @nomcebo_zikode kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika haya kufuatia video hiyo kugonga views Milioni 500.


"Ukuaji wa wimbo huu bado unanishangaza hadi leo. Nimesafiri katika nchi nyingi ambapo bado unachezwa kama vile umetolewa wiki iliyopita! Tunamshukuru Mungu 🙏🏽 #Jerusalema 500 Million views 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger