6/21/2022

Wanafunzi 4 Wafariki Baada ya Ajali ya Boda Boda na Lori Mapinga, Mwanafunzi Aliekuwa Anaendesha Boda Aliwabeba Mshikaki Wenzake Watatu

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Wanafunzi wanne wamefariki Dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugongwa na Lori, katika kitongoji cha Kihara kata ya Mapinga wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.


Akizungumza na TimesDigital mwenyekiti wa Kitongoji cha Kihara Simon Kilian amesema, ajali hiyo ilitokea juzi jioni ambapo Pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na mmoja wa wanafunzi hao, iligonga kingo ya Barabara na Wanafunzi hao kuangukia barabarani hali iliyosababisha kukanyagwa na lori hilo.


“Wanafunzi walipoangukia Barabarani Lori lilikuwa katika mwendo kasi na kuwakanyaga, na hawa wanafunzi waliweza kutambulika kwa sababu mmoja aliazima Pikipiki ndipo mwenye Pikipiki akawajulisha wazazi wa wanafunzi hao.” Alisema Kilian.


Mwenyekiti Kihara amesema mara baada ya tukio hilo miili ya wanafunzi hao ilipelekwa kituo cha afya Karage, na baadae wazazi walifika ili kuitambua miili hiyo, baada ya wazazi kuitambua miili ya watoto wao ililazimika kuwazika kutokana na hali zao kuwa mbaya.


Katika hatua nyengine Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Gregory Mushi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger