6/22/2022

Wananchi wengine Ngorongoro waomba wasiende Tanga

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Serikali imeridhia maombi ya baadhi wananchi wanaohama kwa hiari yao kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika maeneo mengine tofauti na Kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Hayo yamesema na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana, wakati akizungumza  kwa njia ya mtandao kwenye mkutano wa kujenga uelewa kuhusu zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika Pori Tengefu la Loliondo na zoezi la uhamaji wa hiari la wakazi wa Ngorongoro

"Serikali yetu sikivu chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, inaendelea kujali maslahi ya wananchi kwa kutoa uhuru kwa wananchi walioamua kuhamia maeneo mengine kwa hiari yao,"amesema Waziri Chana

Waziri Balozi Dk. Chana amesema ni ruhusa kwa wakazi hao kuchagua kwenda kuishi mahala wanapoona panafaa kwa kufuata taratibu zilizopo bila kuvunja sheria za nchi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger