6/15/2022

Wanatafutwa Washiriki wa 'Squid Game'

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

  


Mtandao wa Netflix upo kwenye mchakato wa kuanza kutafuta washiriki wa kipindi cha TV ambacho maudhui yake yametokana na filamu maarufu ya 'Squid Game' ya Korea Kusini.


Lakini katika kipindi hiki cha Netflix hakutakua na hatari yoyote itakayopelekea kifo kwa mshiriki kama ilivyokuwa katika filamu ya 'Squid Game' ambapo washiriki walishindana na kuuana wenyewe kwa wenyewe.


Mchezo huu utahusisha washiriki 456 kutoka nchi mbalimbali duniani, atakayeshindwa atarudi nyumbani mikono mitupu na mshindi atapewa kiasi cha dola milioni 4.56 sawa na Tsh bilioni 10.


Mshiriki lazima awe na umri kuanzia miaka 21, ajue kuongea kiingereza na awe na muda wa wiki 4 kwa ajili ya kushiriki katika kipindi hicho.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger