Ticker

6/recent/ticker-posts

Wawili Wadakwa kwa Kujiuza Mtandaoni
Wasichana wawili, Marry Sibora (23) na Zainabu Omary (23), wamekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, kwa tuhuma za usambazaji wa picha za ngono na kuuza miili yao kwa njia ya Mtandao.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo amesema watuhimiwa hao ni wakazi wa maeneo mawili tofauti jijini Dar es Salaam ambapo Marry Samson Sibora maarufu kama Asha Zungu ni mkazi wa Sinza Mugabe na Zainabu Yahaya Omary maarufu kwa jina la official Manka ni mkazi wa Buguruni.

Amesema, watuhumiwa hao tayari wameshahojiwa na taratibu za kisheria zinakamilishwa ili waweze kufikishw Mahakani.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kisheria, linatoa onyo kali kwa watu wanao jihusisha na uhalifu kwa njia ya mtandao na njia nyingine, kuwa Serikali na vyombo vyake imejipanga kupambana na uhalifu wa aina yoyote,” amesema Kamanda Murilo.


Watuhumiwa hao wamekamatwa na timu maalum ya Kuzuia na Kupambana na Khalifu Mtandaoni, iliyofanya oparesheni maalum kuanzia May 18 hadi June 26, 2022.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments