Yanga Yamaliza Ligi Kibabe, Mayele Akishindwa Kutetema Kiatu Cha Dhahabu


WINGA wa Yanga, Denis Nkane ametumia miezi minane kufunga bao kwenye mechi za Ligi kuu Bara baada ya kuwatungua Mtibwa Sugar, Yanga ikiibuka na ushindi wa 1-0.

Nkane ambaye amesajiliwa na Yanga dirisha dogo la usajili mara ya mwisho kufunga bao ilikuwa ni Desemba 21 akiwa na Biashara United kwenye mchezo dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Ilulu.

Kwenye mchezo wa leo Nkane ameifungia bao la ushindi Yanga dakika ya 80 akipokea pasi kutoka kwa Yassin Mustafa ambao wote wameingia wakitokea benchi.

Bao la Nkane liliwaamsha Yanga na kucheza pasi za haraka haraka kuelekeza lango la wapinzani wao lakini hazikuwa na madhara langoni kwa wapinzani kutokana na ukosefu wa umakini kwa Herietie Makambo ambaye ametengenezewa nafasi na kushindwa kuzitumia.

Wakati Yanga wakipata ushindi huo mshambuliaji wao kinara wa mabao ameshindwa kuondoka na kiatu cha dhahabu baada ya kuzidiwa na George Mpole wa Geita Gold aliyemaliza na mabao 17.

Mayele amemaliza na mabao 16 na asisti tano huku mpinzani wake George Mpole akifunga bao la 17 na kumuacha bao moja mshindani wake.

Yanga walianza kwa kuliandama lango la Mtibwa Sugar lakini washambuliaji wao walikosa umakini hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna aliyeona lango la mwenzake.

Mtibwa Sugar pamoja na kuhitaji pointi tatu muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kubaki msimu ujao Ligi Kuu waliingia kwa kujilinda kwa kuanzisha wachezaji watano wenye asili ya kuzuia.


Walikuwa wanajilinda zaidi na kutumia mipira mirefu kushambulia kwa kushtukiza lakini hawakupata nafasi ya kumpa mikiki mikiki Mshery ambaye alikaa lango la Yanga.

Yassin kaingia kuchukua nafasi ya Bryson na Moloko katoka kaingia Denis Nkane pia alitoka Dickson Job aliingia Chico Ushindi.

Kwa upande wa Mtibwa walitoka Zigamasabo, Jaffar Kibaya aliingia pia walimtoa Omary Sultan kaingia Ismail Muhesa, Mayanja katoka Hilika.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad