Ticker

6/recent/ticker-posts

Ahmed Ally aibeza jezi mpya Young Africans

 


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally ameibeza Jezi mpya ya nyumbani ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans, baada ya kufanyiwa uzinduzi jana Alhamis (Julai 28), jijini Dar es salaam.

Young Africans ilizindua jezi tatu maalum za msimu ujao 2022/23 (Nyumbani, Ugenini na Chaguo la tatu), huku wengi wakisifia jezi hizo, na baadhi ya wadau wakibeza.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya Kijamii kubeza jezi ya nyumbani ya Young Africans ambayo imenakshiwa na mfano wa picha za baadhi ya alama maalum zilizopo kwenye mikoa ya Tanzania.

Ahmed ameandika: Nimevumilia nimeshindwa acha tu niseme NI MBAYAAA.

Vaa lakin ukijua kuwa umevaa kitu kibayaaaaa na ukivaa unanyata.

Na Sidhani kama KAF watakubali Uniform zenye miundombinu maana nimeona mpaka machinjio ya Vingunguti na Dampo la Kinyamwezi.

Ni mbayaa mpaka aibu tunaona sisi.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments