Ticker

6/recent/ticker-posts

AJALI..Maduka Yateketea Kwa Moto Njombe

 


Takribani maduka sita yameketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Julai 17, 2022, katika eneo la National Housing Njombe mjini na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara.


Hadi sasa chanzo hakijafahamika huku mitazamo ikitofautiana kwa mashuhuda ambao baadhi wakisema kiini cha moto huo ni hitilafu ya umeme na wengine wakidai huenda mlipuko wa gesi ndiyo chanzo.


Mbali na kukumbwa na janga hilo wakati wa uokozi wameibuka vibaka na kuiba mali zikiwemo simu jambo ambalo serikali imetoa onyo na kuahidi kuwasaka wahusika wote walioiba mali za wafanyabishara usiku wa manane.


Kufuatia janga hilo kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Njombe imelazimika kufika eneo la tukio ikiongozwa na mkuu wa wilaya Kissa Gwakisa Kasongwa, na pole kwa wahanga wa janga hilo na hatua zinazokwenda kuchukuliwa na serikali

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments