Ticker

6/recent/ticker-posts

Akutwa na Bangi Tani Moja Kigoma

 


Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Lije Nicholaus  mkazi wa wilaya Kasulu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Bangi inayokadiriwa kuwa na uzito wa Tani mojaKamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi Ramadhani Kingai amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji cha kabulanzwili kata ya Kurugongo ikiwa ni sehemu ya operesheni ya jeshi hilo kudhibiti matumizi biashara ya madawa hayo.


Katika hatua nyingine jeshi hilo kupitia opeshesheni zake  katika kipindi cha kuanzia tarehe kumi mwezi huui limefanikiwa kukamata watuhumiwa watuhumiwa themanini na tano yakiwemo ya mauaji, Ubakaji, na uhamiaji haramu.


Kamanda Ramadhani Kingai amewataka wakazi wa mkoa wa Kigoma kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapohisi ama kubaini uwepo wa watu wanajihusisha na uhalifu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments