Ticker

6/recent/ticker-posts

Aliyemchoma Moto Mke Wake Live Kwenye Tik Tok Hadi Kufa Anyongwa Hadi Kufa


Mwanaume mmoja nchini China amenyongwa leo kwenye kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumchoma Mke wake moto hadi kufa huku akimrekodi video kupitia mtandao wa TikTok.

Tang Lu alimchoma moto mke wake wa zamani Septemba 2020 huku akirekodi moja kwa moja tukio hilo la kikatili jambo lililopelekea mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 kufariki kutokana na majeraha aliyoyapata wiki chache baadaye.

Mahakama katika eneo hilo imetoa taarifa yake fupi siku ya leo kwamba imetekeleza hukumu hiyo ya kifo cha Tang Lu japokuwa Tang alikuwa amekata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kifo lakini akashindwa January mwaka huu.

Kesi hiyo iliyozua shutuma nyingi na hasira nchini China kutokana na matukio ya kikatili wanayokumbana nayo Wanawake katika ndoa zao.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments