Ticker

6/recent/ticker-posts

Aunt: Kusah na Ruby Mbona Freshi Tu, Wala Sihitaji Kiki
AUNT Ezekiel; ni mwanamama nembo ya Bongo Movies na mjasiriamali ambaye anasema kuwa, anawashangaa watu wanaojiuliza kwa nini alimchagua msanii wa kike wa Bongo Fleva, Ruby kwamba ndiye anafaa kufanya kolabo na Kusah ambaye ni baba mtoto wake na amezaa nao wote wawili.


Aunt Ezekiel ameolewa na Kusah

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Aunt anasema kuwa, kusema Kusah aimbe na Ruby alimaanisha kabisa kwa sababu Ruby ni msanii anayeimba vizuri na ana sauti nzuri, anajua wazi kama ni wimbo, basi utakuwa ni mzuri mno.


Ruby amezaa mtoto mmoja na Kusah

“Nilijibu komenti kwa Baba Nono (Kusah) nikimaanisha kabisa siyo kwamba nilikuwa natania au natafuta kiki, hapana na ukweli ndiyo huo kwamba Ruby ni msanii mzuri sana,” anasema Aunt ambaye amezaa mtoto mmoja na Kusah na Rubby amezaa mtoto mmoja na Kusah pia.

 

Cc; @sifaelpaul

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments