Ticker

6/recent/ticker-posts

Baada ya Kutimiza Umri wa Miaka 20 Paula Asema Sasa Akili Imekaa Sawa

 


PAULA Paul Mathyasse almaarufu Paula Kajala; ni binti wa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja au Mama Pau ambaye anasema kuwa, akili yake imekua na ana mipango mingine mizuri kwa maisha yake ya mbeleni.


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Paula ambaye jana  (Ijumaa) ametimiza miaka 20 na anazindua duka lake rasmi la kuuza nguo, anasema kuwa hiyo ndiyo hatua moja kubwa ambayo ameipiga na mambo mazuri zaidi yatakuja na wale wanaomfikiria tofauti watajua.


“Najua kuna watu wananichukulia tofauti sana, lakini hata mimi nina mipango yangu mizuri ya maisha yangu kama msichana ninayekuwa na ninayeendelea kukua na akili imenikaa sawa wawia,” anasema Paula ambaye ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti).


 

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments