Ticker

6/recent/ticker-posts

Barnaba Amjibu Joslin Baada ya Msanii Huyo Kulalamika Nyimbo zake Kuimbwa na Wasanii Majukwaani Bila Yeye Kupata Kitu


NIITE BASI ni moja ya hit songs zilizo muweka @joslin_tz kwenye ramani ya Bongo Flava kwa ukubwa hapo zamani na ni Identify yake hadi leo popote pale atapo shika maiki, mkongwe huyo na member wa kundi la muziki la Wakali Kwanza, hivi karibuni amefanya interview kwenye moja ya media na bila kutaja majina, akalalamika wasanii kutumia nyimbo zake kwenye majukwaa wanapo fanya shows, wakati wasanii hao wakilipwa, msanii huyo amelalamika yeye hapati chochote kitu. Hivi karibuni msanii @barnabaclassic ni miongoni mwa wasanii walio tumia wimbo wa NIITE BASI kwenye jukwaa.


Akibonga na @soudybrown kwenye U-HEARD, Barnaba amedai hajawahi mkosea heshima Joslin na hajawahi imba nyimbo zake kwa malengo ya kupata pesa, maana yeye kama Barnaba anajitosheleza kwa kuwa na ngoma nyingi tu ambazo ni hits na anaweza ziimba kwenye shows na watu wakaenjoy, ila ifike hatua Joslin aelewe sometimes wasanii kuimba nyimbo za wasanii wengine ni kama recognition na kuheshimu talents za wasanii hao.


Mopao ameendelea akidai kuwa, amewahi fanya back vocal kwenye majukwaa ya Fiesta Wakali kwanza walipokuwa wakiperform tena kwa mapenzi mazito,sababu ni miongoni mwa wasanii anao wakubali, amewahi ongea mara kadhaa kuwa ni shabiki mkubwa wa Joslin, hasa iweje leo alalamike kitu kama hiki, mbona nyimbo za kina Westlife zinaimbwa kwenye majukwaa hapa Bongo, ina maana wasanii wana copyright na hizo Kazi? au wanawalipa hao Westlife?, Jibu ni Hapana, bali ni mapenzi tu.


Hii sio mara ya kwanza kwa mkongwe Joslin kulalamika kuhusu wasanii wa sasa, hivi karibuni alipita na @maarifabigthinker akimtaka awe anamtaja kama kamuinspire anapotumia nyimbo zake.😀

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments