Ticker

6/recent/ticker-posts

Chanzo cha Kupigwa Rasasi Hadi Kufa Mfanyabiashara Tabora Chatajwa


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio la mauaji ya Mustapha Mohammed (36) Mfanyabiashara Mkazi wa Ipuli kata ya Mpela manispaa ya Tabora aliyepigwa risasi akiwa anaendesha pikipiki.


ACP Abwao amesema chanzo cha kupigwa kwake risasi wakati akiendesha pikipiki kwenda kwenye biashara zake ni ugomvi wa kibiashara ambapo Watuhumiwa na Marehemu walikuwa wakidaiana.


“Walimfukuzia na kumpiga risasi kwenye sehemu ya ubavu wa kulia kwakutumia bunduki aina ya gobore ambayo imetengenezwa kienyeji na ilipatikana eneo la tukio” 

Polisi Tabora wamesema wamewakamata Watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya Mfanyabiashara Mustapha Mohamed (36) ambaye alipigwa risasi ya ubavuni akiwa anaendesha pikipiki chanzo kikidaiwa ni ugomvi wa kudaiana kibiashara, Mtuhumiwa wa tatu anasakwa


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments