Ticker

6/recent/ticker-posts

Diamond Platnumz Anauwezo Kuwasaidia Wasanii wa BONGO Kutoboa Nje zaidi ya Anachokifanya Sasa Hivi, Hajaamua tu


Neno Kupeperusha Bendera ya Taifa” ni pana kidogo, Sanaa haihitaji mtu mmoja pekee kujulikana nje ya mipaka ya Tanzania, tunahitaji kuwa nao wengi, ila kabla hatujawanyoshea vidole wasanii hawa ambao wanalitafuta soko la kimataifa, hivi huyu mmoja mwenye matamanio ya kuona hata akifa leo bado bendera ya Tanzania itabaki kwenye list ya wasanii 10 Afrika wenye ushawishi duniani, anafanya jitihada gani kwa wasanii wenzie?.


Najua utimu unamaliza sana tasnia ya muziki, alafu tunajiroga wenyewe na kuhitisha mikutano ya kutafuta wachawi wa hii sanaa, kumsaini mtu kwenye Label si msaada na haitoshi kusema umesaidia, si kila msaada lazima ukurudishie malipo. Tunamsema DIAMOND, maana ndiye msanii pekee toka Bongo ambaye kwa sasa ana mabawa ya kupaa umbali mrefu zaidi nje ya mipaka ya Bongo kuliko wasanii wengine.


Tunakumbuka alicho kifanya BURNA BOY kwa REMA, RUGER na OMAH LAY August 2021, kuwabeba toka Nigeria na kuwapandisha kwenye show yake kwa mara ya kwanza pale o2 Arena Uingereza, DIAMOND anashindwa nini kumshtua MARIOO ajiandae maana anaenda kumpandisha kwenye jukwaa la Afronation, Mbona MALUMA aliweza kumpandisha RAYVANNY kwenye majukwaa makubwa mara 3,kwani alishindwa Mama Tetema kuimba mwenyewe? By the way Marioo ni mfano tu ila tuna wasanii wengi ambao naamini kama outsiders watawajua basi itakuwa ni hatua kubwa sana kwao.

AJIRA ZAIDI YA 100...Jiunge na GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO> HAPA

Tukitoka nje tunarudi home kujiliza kama ROMY JONS, kwanini tuna msanii mmoja kimataifa, Ni UNAFIKI MKUBWA, Diamond ana uwezo wa kuwasaidia wenzie kwa njia hii ila ukweli ni kuwa Bongo kuna umimi, sio muziki tu, sehemu nyingi watu wanaminyiana nafasi kitu ambacho si mchongo. Alafu utasikia shabiki wa mchongo anakwambia kwani yeye alisaidiwa na nani?😁, hatuwezi kuwa sawa, Magap lazima yawepo.


By Sajo

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments