Ticker

6/recent/ticker-posts

Diamond Platnumz Asema Hajutii Kuchukua Asilimia 60% ya Mapato ya Wasanii wa Wasafi

 


Diamond amejibu madai ya kunyonya wasanii wake, amesema kwa Harmonize na Rayvanny peke yao alipowasaini uwekezaji kwao ulimgharimu zaidi ya milioni 600 za Kitanzania


Mond ameongeza kuwa karibia wasanii aliowasaini walikuwa katika lebo mbalimbali kabla na hawakuwa maarufu wala wenye mafanikio katika lebo hizo hadi walipokaribishwa Wasafi uwekezaji mkubwa ndio ukafanywa kuwanoa kibiashara wauzike sokoni hivyo yeye ni mfanyabiashara anawekeza pesa zake nyingi zirudi na faida pia


Amesema maneno maneno au mabifu yanaanza pale msanii anataka kujitoa na kutakiwa kulipia fidia za mikataba ya uwekezaji ulioigjarimu Wasafi pesa nyingi. Kiufupi Diamond anamaanisha kuwa yeye hatoi msaada kwa wasanii bali anawekeza kibiashara katika biashara ya muziki


Ukiachana na hayo, kumbukumbu pia zinaonesha kipindi hicho Diamond Platnumz na yeye wakati alipokuwa akisimamiwa na kina Papaa Misifa aliwahi kuripotiwa kuutengua mkataba ambapo Diamond aliripotiwa kukubali kulipa pesa ya fidia kwa kuvunja mkataba husika baada ya kuona mkataba hauna kasi ya kumpeleka anapopataka kimuziki. Na baada ya hapo Diamond ndio akaanza kufanya kazi na kina Babu Tale na Sallam Sk

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments