Dkt. Cheni: Harusi ya Nandy na Billnass Mimi Nilimshinda kwa Kura MC Gara B

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPAMSHEREHESHAJI maarufu nchini na Staa wa filamu Dkt Cheni amesema dili la kusherehesha harusi ya mastaa wa Bongo Fleva Billnass na Nandy alipewa yeye baada ya kufanyika mchakato wa kupigiwa kura ambapo yeye ndiye aliyeibuka mshindi namba moja.

Cheni ameyasema hayo wakati alipofanya mahojiano ndani ya Studi za Global TV na Global Radio ambapo amedai kuwa yeye alikuwa namba moja na mpinzani wake wa karibu alikuwa MC Gara B ambaye yeye alilazimika kupewa dili la Send Off ya Nandy ili kuhakikisha sherehe hiyo inakuwa kubwa na kufana.


Sherehe ya Harusi ya Billnass na Nandy ilishereheshwa na Dkt Cheni
Dkt. Cheni amebainisha kuwa yeye hakuomba dili hilo lakini kutokana na ukubwa wake alikuwa akipigiwa simu nyingi kutoka pande zote mbili kwa maana ya upande wa mwanamke ambaye ni Nandy na kwa upande wa mwanaume ambaye ni Billnass ambao wote kwa pamoja walimsihi akubali dili hilo kwani walikuwa na Imani naye kutokana na ukubwa wake.

“Upande wa kina Nandy na upande wa kina Nenga walikuwa wanashirikiana kwamba Send Off afanye nani harusi afanye nani kwahiyo wkaafanya mchakato mchakato Send Off wakaona wampe jamaa mimi nifanye harusi, hayo ni maamuzi ya kwao, kwahiyo walinipigia simu wakaniomba ofcourse simu zao zilikuwa nyingi mara unapata simu kutoka kwa Nandy mara unapata kutoka kwa Nenga.” Amesema Dkt Cheni.


 
Mara nyingi kumekuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashabiki na watu mbalimbali wakiwashindanisha washereheshaji wawili Dkt Cheni pamoja na MC Gara B ili kujua ni nani MC Mkubwa nchini.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad