Ticker

6/recent/ticker-posts

Doreen Lyatonga Mrema "Mzee Mrema Ananifikisha Hatari, Hatuachani"Doreen Agustino Mrema ambaye ni mke wa mwanasiasa maarufu nchini,Agustino Lyatonga Mrema ameeleza kufurahia maisha ya ndoa na mmewe baada ya mwanasiasa huyo kumpoteza mke wake mpendwa Rose Mrema Mwaka huku akisisitiza mmewe anamridhisha kila kona.


Akizungumza na Vyombo Vya habari Doreen amesema anafurahia ndoa aliyoifunga na mwanasiasa huyo kwa kuwa Mzee Mrema anamtimizia majukumu yote na kumtosheleza likiwemo tendo la ndoa tofauti wanavyo fikiria watu wengine kwamba mume wake hawezi kumtosheleza kiunyumba .


Doreen ameleza kwamba tuhuma zilizo sambazwa mtandaoni kwamba amedai talaka kwa mume wake na wameanza kufarakana si za kweli na kupotosha umma kwa kuwa tamgu aolewe na mwanasiasa huyo wamekua na mapenzi mazito na wanafurahia ndoa yao kama Vijana walioko katika uchumba


"Mrema ni Mume wangu nampenda sana kwa dhati siwezi kumwacha wala mimi sijadai talaka kwake bali ni baadhi ya mitandao inapotosha kwamba mzee wangu hawezi kuniridhisha katika ndoa jambo ambalo sio kweli "


"mimi nipo katika ndoa naenjoy sana penzi la Mume wangu Mrema kwani anayejua utamu wa ndoa ni Mimi sikiliza Mzee anaweza shughuli mpaka mimi mwenyewe najiuliza ni yeye kweli au maana ananitosheleza vya kutosha siwezi kumwacha Mrema yaani nina enjoy kupitiliza amekua kijana na anafanya mazoezi ya kujiweka vizuri kiavya Alisema Doreen " Bila aibu huku akionyesha tabasamu zito .


Hivi karibuni kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii kumezuka na taarifa zikimlenga mke wa Mrema Doreen kwamba ameomba Talaka ya kuachana na Mzee Mrema mara baada ya kupita Miezi Minne kufunga Ndoa yao huko kjjijini kwao Kiraracha Mkoani kilimanajaro kwa madai kwamba Mzee Mrema ameshindwa kumridhisha Mrembo huyo hususani katika tendo la ndoa .


MwanaDada huyo amekanusha vikali taarifa hizo na kusema maneno hayo katu hayatamfanya amuache Mme wake Mrema kwa kuwa anampenda kwa dhati kutoka Moyoni mwake na mpaka sasa hajaona kasoro yoyote kutoka kwa mume wake .


Ameeleza kwamba kwa sasa anafurahia ndoa yake na wamejiwekea utaratibu wa kwenda mazoezi kwa pamoja na sasa wamehamishia makazi yao Sala Sala Mkoani Dar es Saalam ambapo mme wake anaendelea na majukumu ya siasa huku akiendelea kumlea asipate changamoto yoyote kutokana na umri wake kusogea .


Mrembo huyo ameapa afe beki afe kipa hawezi kuomba talaka kwani hakuna aliyemlazimisha kuolewa na Mrema na kuhusu kwamba hatosheki katika ndoa yake sio kweli kwa kuwa Mrema amekuwa akimpatia mapenzi mazito na haoni sababu ya kudai talaka .


Kwa upande wa ndugu zake Doreen walisema taarifa hizo ni za uzushi kwani mara kwa mara wamekua na tabia ya kumjulia hali mtoto wao pamoja na mume wake na hawajakutana na malalamiko ya aina yoyote kutoka kwa Mrema akilalamikiwa na mke wake kwamba hawezi tendo la ndoa na kuwataka wananchi kuzipuuza habari hizo.


Kwa upande wake Mrema alifunguka kwamba tangu ampoteze Mke wake Rose Mrema amepata faraja kwa Doreen namna anavyomjali na kumpa mapenzi motomoto huku akisisitiza wanamuonea wivu huku akisisitiza humtosheleza mkewe mpaka kuna muda humwambia tupumzike kidogo .


"Mimi nawaambia Doreen namtosheleza kwani umesikia wapi n'gombe anazeeka maini mimi ni jogoo la shamba nawika mpaka mjini waache wivu nishawapiga bao watafute kiki kwingine mimi na Doreen tushapendana haachwi mtu hapa " alisisitiza Mrema


Mwisho.....

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments