Ticker

6/recent/ticker-posts

Esma Khan: Hatujui Penzi la Diamond Platnumz na Zuchu, Amtaja Aaliyah
UKISIKIA jina la Esma Khan, kama wewe si mdau wa mitandao ya kijamii Bongo, unaweza kusitasita kidogo na kudhani huwenda ni jina la muigizaji kutoka India lakini ukweli ni jina la Kibongo kabisa.

Kwa wafuatiliaji wa muziki wa Bongo Fleva na habari za mastaa Bongo, bila shaka watakuwa wanaijua familia ya staa wa muziki huo, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz na katika familia hiyo yupo Esma Khan ambaye ni dada yake.

Huwezi kumkuta Esma akiigiza au kuuza sura ‘video queen’ kwani alishaufanya hivyo kipindi hicho kaka yake anatoka kimuziki katika Video ya Wimbo wa Kamwambie.


Staa wa muziki, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz akiwa na Zuchu.
Esma Platnumz ametokea kujipatia umaarufu mkubwa kwa kuwa ni memba wa familia ya Diamond ambayo hufuatiliwa na mashabiki wengi. Ijumaa limemfungia safari hadi dukani kwake, Sinza-Afrikasana jijini Dar na kufanya naye exclusive Interview ambapo Esma anasema kuwa hana wifi yeyote ambaye amezaa na kaka yake ambaye anambagua kwa sababu ukweli ni kwamba hajui atafia wapi wala kuzikwa wapi hivyo wote ni wifi zake na anawapenda kwa sababu wameongeza familia yao.


 
Esma ambaye hutazamwa mno na wananzengo kila afanyalo anasema kuwa, japokuwa kaka yake ni maarufu, yeye kamwe hawezi kujibweteka na kusubiri pesa za kaka yake, badala yake anapambana mwenyewe.

IJUMAA: Habari Esma, mzima? Naona unazidi kupendeza tu…

ESMA: Kwa kweli sina stresi kwenye kichwa change. Kwa nini sasa nisipendeze mimi? Na pia najua kuitafuta pesa.


IJUMAA: Biashara naona inazidi kukua tu siku hadi siku, umewezaje? Kwa sababu imekuwa ngumu sana kwa mastaa mbalimbali?

ESMA: Ukweli kazi hii ndiyo kila kitu kwenye maisha yangu, inasomesha watoto, inalisha na kila mtu unaiheshimu sana, unajua kuna wengine nyota za biashara hawana kabisa.

IJUMAA: Lakini pia kila siku unakaa dukani kitu ambacho kiliwashinda wengi, hii vipi?

ESMA: Sasa nisipokaa dukani nitakaa wapi miye maana dukani ndipo kazini kwangu na uzuri kabisa mimi siyo mzururaji, dukani ndiyo sehemu yangu ya kazi yangu.


 
IJUMAA: Esma sijawahi kuona una rafiki yule wa damu wa kuongozana kule na kule, hii vipi?

ESMA: Rafiki yangu mkubwa ni mama yangu, kwa kweli ndiye mtu wangu wa karibu sana na kingine ndiye rafiki wa kweli kwangu, kutwa tupo wote.

IJUMAA: Hujamisi ndoa yako Esma?

ESMA: (khaaaaa) naimisije kwanza kwa sababu mimi nimeshaolewa sana ujue (mara nne) kwa hiyo hakuna cha kunikumbusha chochote.

IJUMAA: Sasa kwenye upande wa mawifi mpaka sasa haijajulikana ni nani unampenda?


ESMA: Mimi kiukweli mawifi zangu wote ninawapenda sana, maana mimi mwenyewe sijui nitafia wapi, Nairobi, South, Tanzania au Uganda? Hivyo wote ambao wana watoto na kaka yangu, nawapenda.

ESMA: Vipi kuhusu Zuchu? Ninamaanisha kuhusu uhusiano wake na Diamond?

ESMA: Yaani ukweli hatuna tunachojua kama kuna uhusiano wa kimapenzi unaoendelea, mimi najua ni mtu na bosi wake tu na si vinginevyo.


Aaliyah mtangazaji wa Wasafi.
Ijumaa: Mbona kama wanaweka wazi sana sasa hivi?

ESMA: Hapana, yule ni mtu na bosi wake tu, hakuna uhusiano.


 
IJUMAA: Na kuhusu Aaliyah, maana naona ni marafiki na pia ilidaiwa alikuwa na uhusiano na Diamond?

ESMA: Watu wanachanganya mambo sana tena sana, Aaliyah mimi jirani yangu; yaani nimejikuta tumepanga nyumba sehemu moja. Kifupi mwenye nyumba wetu mmoja ndiyo hivyo siyo kingine, kwa hiyo hata kumualika kwenye vitu vyangu kwa sababu ni jirani.

IJUMAA: Vipi kuhusu jina la Yuda, naona limepotea kabisa?

ESMA: Unajua mimi siku zinavyozidi kwenda ndiyo mambo yanabadilika hivyo kuna vitu nilivipunguza kwenye mitandao na ndiyo maana unaona hata hilo jina la Yuda lilijifia.

IJUMAA: Wengi walidhani kuwa labda umempata mtu amekuzuia?

ESMA: Mtu gani wa kunizuia mimi jamani, mbona hayupo.

IJUMAA: Lakini nasikia una uhusiano mwingine sasa na Coy Mzungu?

ESMA: Hebu nicheke miye, yule mshikaji sana tena sana na si kingine kabisa.

IJUMAA: Unajua watu wengi wanajua wewe ni boss lady kwa sababu ya kaka yako, hilo limekaaje?

ESMA: Pesa za Nasibu (Diamond) haziwezi kuwa zangu, anayekula pesa zake kila siku nasema ni mama yake na hilo liko wazi na hata kama kunisaidia, ameshanisaidia na kuniinua mpaka hapa sasa nilipofikia.

IJUMAA: Nashukuru sana kwa muda wako.

ESMA: Karibu tena na tena.Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments