Ticker

6/recent/ticker-posts

Esma Platnumz Adokeza Juu ya Suala la Kujaribu Ndoa kwa Mara Nyingine
ESMA Khan au Esma Platnumz; ni mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholati) na dada wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye amedokeza juu ya suala la kujaribu ndoa tena, miaka miwili baada ya ndoa yake na mfanyibiashara Msizwa kuvunjika.

 

Esma ambaye ni mfanyabishara wa vitambaa aliolewa mke wa tatu na Msizwa ambaye ni Mtanzania anayepiga madili yake nchini Afrika Kusini ambapo ndoa yao iligharimu shilingi milioni 300 kabla ya kuvunjika ndani ya miezi mitatu ya awali.

 

Sasa, Esma anasema kuwa, tayari ana mchumba ambaye anatarajia kuingia naye kwenye ndoa kwa mara nyingine; hii itakuwa ni ndoa yake ya nne.

 

“Ndiyo, niko kwenye uhusiano na naolewa tena Lakini uhusiano wangu hivi sasa siyo wa mitandao ya kijamii kama hapo awali,” anasema Esma ambaye ni mama wa watoto wawili kutoka kwa baba tofauti.

 

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments