Ticker

6/recent/ticker-posts

Haji Manara Alia na Uwizi wa Jezi Ataka Simba na Yanga Ziungane "Haiwezekani Maaramia Kufaidika"
Ameandika Haji Manara:

"Tunaweza kushindana ndani na nje ya Uwanja kwa nguvu kubwa, tunaweza kupambana Usiku na Mchana kusaka Saini za Wachezaji wapya wa kuja kututumikia, Tunaweza kutaniania vilivyo hadi kushikana mashati, tunaweza hata kushtakiana pengine kwa mambo Ya kawaida tu, yasio na mbele wala nyuma.

Lakini Yanga na Simba tuna Common Interest hususan katika Mapato ya Vilabu vyetu, tunao Wajibu mkubwa wa kushirikiana na kutafuta Solution ya Jambo kama hili.

Haiwezekani Maharamia wafaidike na sisi tunaendelea kupingana tu,tutafute namna ya kushirikiana na Mamlaka kupunguza Wizi huu kama sio kuumaliza kabisa.

Ikiwa Zamalek na Ahly ambao ni Mahasimu wakubwa,wanashirikiana inapokuja issue ya mapato, Sisi ambao ni Watani tu Wa jadi tunashindwaje?

Barcelona na Madrid ni Maadui kabisa lakini when it comes kwenye Revenue, wanakaa pamoja kulinda ukubwa wao na biashara zao zinazowaingizia mapato.

Even Raja na Wydad Casablanca,,Wanafikia hadi kupigana, lakini ikija issue inayowaingizia mapato huwa kitu kimoja.

Huko kote Yanga na Simba hatujafikia,,Sisi ni midomo tu na kucharurana kwingi,,Why tushindwe kutafuta Suluhisho la hawa Vibaka wanaozihujumu hz Clubs ?

Tukae Chini tumalize hili jambo, kulalamika peke yake hakutoshi, hizi tofauti zetu sio lolote mbele ya masalahi ya vilabu vyetu, tunaweza tukiamua.Wenye dhamana ni Washabiki na Wanachama wetu,,Sisi tupo on behalf of them,,tunashindwa vp na hawa wahuni?

Wiki Chache zijazo tunakwenda kuzindua Jezi zetu Mpya, najua Maharamia wamejipanga kuendelea kutupiga, twendeni tukaweka mikakati ya kushinda hii vita kwa pamoja,TUNAWEZA TUKIAMUA

Nb: hii haina Byuti Byuti ni kilio Kwa kweli 😭😭 " Haji Manara

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments